
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Whozu, ameonyesha hisia zake za furaha baada ya mpenzi wake, Wema Sepetu, kujifungua mtoto wa kiume.
Kupitia ujumbe wake, Whozu amesema ujio wa mtoto wao ni uthibitisho kuwa uwezo wa Mungu ni mkuu kuliko matarajio na makadirio ya binadamu.
βSio kuwa tu wazuri sana mbele zake lakini ilimpendeza aonyeshe ukuu wake kwenye uso wa dunia kuwa makadirio ya wanadamu hayawezi kushinda kudra zakeβ¦β
Whozu aliendelea kueleza kuwa tukio hilo ni kibali maalum kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya kipindi kirefu cha maombi na subira.
βHakika Mwenyezi Mungu amejidhihirisha na kutupa kibaliππΌ.β
Katika ujumbe huo, msanii huyo alimpongeza Wema huku akitoa shukrani kwa wote waliokuwa wakiwasapoti na kuwaombea.
βHongeraa shunu wangu na akhsanteni nyote mliokuwa mkituombea. Mungu yupo na wanaomtumaini. Tusichoke kukesha tukiomba maana yeye ni mwenye huruma siku zoteππΌ.β
Ujumbe huo umeibua hisia kubwa kwa mashabiki wengi, hasa kutokana na safari ndefu ya Wema ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mama, huku wengi wakitafsiri tukio hilo kama ushindi wa imani, subira na matumaini.
