Ali Kamwe : Yanga Hatuuzi Ticket za Dadi ya Simba na Yanga
Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema klabu hiyo haina mpango wowote wa kushiriki mechi ya dabi dhidi ya watani wao wa jadi, akisisitiza kuwa haipo kwenye ratiba yao rasmi ya mashindano.
“Tunajiandaa na mechi ya Prisons na Dodoma Jiji, hatupo kwenye hiyo program ya dabi” amesema Kamwe, huku akieleza kuwa tayari idara zote ndani ya klabu zimepewa taarifa rasmi kuhusu mwelekeo huo.
Kamwe pia amesema hakuna tiketi itakayouzwa kwa niaba ya Yanga kwa mechi hiyo kwani, kwa mujibu wa kanuni, klabu inalindwa kisheria dhidi ya hilo.
Ameongeza kuwa Yanga haijapokea maelekezo yoyote kutoka serikalini kuhusu mechi hiyo: “Serikali kupitia Waziri Kabudi alisema haihusiki na dabi, na hatujapokea maelekezo yoyote kutoka kwa serikali.”