Mabosi wa Azam EC wameanza mipango ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao ikielezwa ipohatua ya mwisho kumsainisha mkataba, kipa wa Aishi Manula, sambamba na kumbeba kiungo mahiri aliyekuwa akicheza soka la kulipwa huko Misri.
Taarifa za uhakika ilizopenyezewa Mwanaspoti ni
kwamba, Manula atasaini mkataba mpya leo Alhamisi baada ya jana kufanyiwa vipimo katika hospitali ya Agakhan akiwa sambamba na kiungo Muhsin Malima ambaye naye inaelezwa anajiandaa kusaini mkataba wa kuitumimkia timu hiyo.
Azam FC imemrejesha Manula baada ya kipa huyo kuihama 2017 kujiunga na Wekundu hao ambao hata hivyo kuazia msimu uliopita benchi la ufundi limeonesha kutompa nafasi kikosini.
Mwanaspoti