Aliyepanga Mauaji ya 2PAC Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 40 Jela

Aliyepanga Mauaji ya 2PAC Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 40 Jela
Aliyepanga Mauaji ya 2PAC Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 40 Jela

Aliyepanga Mauaji ya 2PAC Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 40 Jela

Mahakama nchini Marekani imemhukumu Duane “Keffe D” Davis, mwenye umri wa miaka 63, kifungo cha miaka 40 hadi maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mauaji ya Mwanamuziki maarufu wa Rap, Tupac Shakur.

Hukumu hiyo imetolewa Jumanne, Oktoba 13, 2026, mjini Las Vegas, Nevada, baada ya Davis kupatikana na hatia ya mauaji ya daraja la kwanza Agosti 31, 2026, katika kesi iliyochukua takribani miongo mitatu kabla ya kufikia hatua ya hukumu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Associated Press (AP), upande wa mashtaka ulidai kuwa Davis aliratibu shambulio hilo la kutumia bunduki lililotokea Septemba 7, 1996, baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya kundi la Tupac na mpwa wake, Orlando “Baby Lane” Anderson, katika hoteli ya MGM Grand.

Tupac alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lililokuwa likiendeshwa na Marion “Suge” Knight. Mwanamuziki huyo alifariki siku sita baadaye akiwa na umri wa miaka 25. 

Ushahidi uliotumika katika kesi hiyo ulijumuisha maelezo ambayo Davis alitoa katika mahojiano na kitabu chake cha kumbukumbu za maisha, Compton Street Legend, kilichochapishwa mwaka 2019.

Hata hivyo, upande wa utetezi ulipinga madai ya mashtaka na Davis anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. 

Kesi hiyo imekuwa miongoni mwa mauaji yaliyovuta hisia za mashabiki wa muziki duniani kwa karibu miaka 30, huku hukumu hiyo ikiwa ya kwanza dhidi ya mtu aliyeshtakiwa kuhusika na mauaji ya Tupac

Related Posts