
Kesho ya Depu ndani ya Yanga bila shaka yeye mwenyewe hana uhakika nayo kutokana na ujio wa washambuliaji wawili ambao watakuwa na nafasi kubwa mbele yake.
Depu anajua kufunga na nilidhani ndio atakuwa chaguo la kwanza la Yanga lakini kwenye dirisha la uhamisho mambo huwa yanabadilika sana ni ngumu kutabiri nini kinaweza kutokea.
Kwangu Depu anaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa Azam ambao hawajapata striker wa maana kwa muda mrefu sana na haijalishi wamekuwa na dirisha gani nzuri bila namba tisa wa maana ambaye amethibitisha ubora wake ndani ya Tanzania watakuwa kwenye wakati mgumu ni vizuri kwa Feisal Salum kuwa na mtu mwingine wa kumsaidia kufunga tena mshambualiaji namba tisa halisi.
Itakuwa dhambi kwa Depu kuondoka Tanzania hii ukizangatia kupata namba tisa ndani ya Afrika ni changamoto kubwa sana, hata Simba Depu anaweza kuwapa huduma nzuri tu ikitokea ishu ya Selemani Mwalimu na Wydad Casablanca hajapata suluhisho na yeye akabaki basi hata Depu anawafaa Simba kwa sababu ni timu ambayo inatengeneneza nafasi sana ambazo zinajitahitaji target man na Depu kazi hiyo anaiweza vizuri tu
