Dkt. Mwinyi atangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 300,000 hadi TZS 500,000

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 300,000 hadi TZS 500,000 kwa mwezi.

Dkt. Mwinyi ametangaza ongezeko hilo Mei 01, 2026 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutolewa kuanzia Januari 2027.

Aidha, amesema uamuzi huo unaenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuimarisha mazingira ya kazi na kuhakikisha kuwa watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati, huku akitoa wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, juhudi, nidhamu na uzalendo ili kuleta maendeleo endelevu Zanzibar.

Mbali na hayo, Dkt. Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi, na kwamba itaendelea kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kukabiliana na changamoto zote zinazowakabili wafanyakazi nchini.

Related Posts