Yanga Yaingia Kina Kirefu Kumpata Aziz Ki: Yatumia Zaidi ya Sh2 Bilioni Kumng’oa Libya

Yanga Yaingia Kina Kirefu Kumpata Aziz Ki: Yatumia Zaidi ya Sh2 Bilioni Kumng'oa Libya
Yanga Yaingia Kina Kirefu Kumpata Aziz Ki: Yatumia Zaidi ya Sh2 Bilioni Kumng’oa Libya

Yanga Yaingia Kina Kirefu Kumpata Aziz Ki: Yatumia Zaidi ya Sh2 Bilioni Kumng’oa Libya

Klabu ya Yanga imeweka rekodi nyingine kwenye soko la usajili baada ya kutumia zaidi ya Sh2 bilioni kumrejesha kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kutoka Al Ittihad ya Libya.

Ili kufanikisha dili hilo, Yanga ililazimika kulipa Dola 450,000 (takribani Sh1.2 bilioni) kuvunja mkataba wa miaka mitatu aliopaswa kuuitumikia Al Ittihad. Pamoja na gharama hiyo ya klabu, Aziz Ki amekabidhiwa Dola 350,000 (Sh928 milioni) kama dau lake binafsi (sign-on fee) kwa ajili ya mkataba wa miaka miwili aliosaini Msimbazi.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa mazungumzo ya kuvunja mkataba yalikuwa magumu, lakini Yanga ilifanikiwa kuishusha Al Ittihad kutoka Dola 500,000 zilizotakiwa awali.

Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, amethibitisha kukamilika kwa usajili huo mnono akibainisha kuwa mchezaji huyo atatambulishwa rasmi leo katika uwanja wa KMC, huku akijigamba kuwa klabu hiyo haina shida ya kifedha kutokana na usaidizi kutoka kwa mdhamini wao mkuu, GSM.

Related Posts