EWURA Yaingiza Afueni: Bei za Petroli na Dizeli Zashuka Nchini

Bei za Petroli na Dizeli Zashuka Nchini
Bei za Petroli na Dizeli Zashuka Nchini

EWURA Yaingiza Afueni: Bei za Petroli na Dizeli Zashuka Nchini

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za bidhaa za mafuta nchini zinazoanza kutumika leo, Septemba 2, 2026. Katika mabadiliko hayo, bei ya petroli imeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita huku dizeli ikishuka kwa Shilingi 101 kwa lita, hatua inayotajwa kutokana na juhudi za Serikali za kuweka bei himilivu licha ya msukosuko wa soko la dunia unaosababishwa na migogoro ya Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei za rejareja jijini Dar es Salaam zimefikia Sh3,796 kwa lita ya petroli, Sh3,877 kwa dizeli, na Sh3,713 kwa mafuta ya taa. Mkoani Tanga, petroli itauzwa kwa Sh3,872 na dizeli Sh3,953, wakati Mtwara petroli itakuwa Sh3,909 na dizeli Sh3,990. EWURA imewatahadharisha wafanyabiashara wa jumla na rejareja kuzingatia bei hizo elekezi, ikisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka.

ALSO READNini Maana ya Rangi za Shanga Kiunoni mwa Mwanamke Kimapenzi?

Related Posts