
Erling Haaland ameiongoza Norway kutinga robo fainali Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kuifunga Brazil mabao 2-1 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa katikabUwanjabwa MetLife, Marekani usiku wa kuamkia leo Julai 6, 2026.
Haaland alifunga mabao yote mawili katika dakika za mwisho za mchezo, likiwemo bao la kwanza dakika ya 79 kwa kichwa na la pili dakika ya 90 kwa shuti kali lililoipa Norway ushindi muhimu.
Bao la kufutia machozi la Brazil lilifungwa na Neymar kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 100 ya muda wa nyongeza.
Shujaa mwingine wa Norway alikuwa kipa Orjan Nyland, aliyekuwa na kiwango cha juu kwa kuokoa penalti ya Bruno Guimarães kipindi cha kwanza pamoja na kufanya save nyingi muhimu zilizoiweka timu yake kwenye mchezo.
Kwa upande wa Brazil, matokeo hayo yanamaanisha wameondolewa kwenye hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza tangu 1990, huku pia wakiendeleza rekodi ya kutolewa na timu za Ulaya kwa mara ya sita mfululizo kwenye Kombe la Dunia.
Haaland sasa amefikisha mabao saba kwenye mashindano hayo, akilingana na Lionel Messi katika orodha ya wafungaji bora wa mashindano.
Norway sasa itakutana na mshindi wa mchezo kati ya England na Mexico katika robo fainali
