
Habari njema kwa Yanga na mashabiki wake ni kuwa kiungo wao wa zamani Stephane Aziz Ki amekubali kurejea Jangwani
Ki ambaye aliuzwa katika klabu ya Wydad Athletic akitokea Yanga na hatimaye kujiunga na klabu ya Al Ittihad ya Libya akiuzwa kwa dola 300,000 sasa anataka kurejea Jangwani
Aziz Ki amewasiliana na rais wa klabu ya Yanga Injinia Heris Said na kukubaliana baadhi mambo ili dirisha la usajili litakapofunguliwa aweze kutua, imefahamika
Tangu kuondoka kwa kiungo huyo mshambuliaji Yanga haijaweza kupata mbadala wake mpaka sasa licha ya kwamba Allan Okelo anajitahidi katika nafasi hiyo lakini anaenjoy zaidi kucheza pembeni
Mpaka sasa Yanga ina uhakika wa kushiriki ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao hivyo inahitaji kuwa na wachezaje wazoefu na wenye viwango bora kama Aziz Ki.
