Afisa habari wa zamani wa vilabu vya Simba Sc na Yanga Sc Haji Sunday Manara amezua gumzo zito kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kutupa kijembe kizito kwenda kwa watani zake wa jadi yaani Simba Sc.

Haji Manara ni moja kati ya wadau wa soka ambao wameonyesha kufurahishwa sana na kitendo cha Simba Sc kupoteza mchezo wao wa wa nusu fainali ya michuano ya CRDB Federation Cup waliocheza siku ya jana Jumamosi tarehe 31 Mei, shidi ya klabu ya Singida Black Stars katika dimba la Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara.

Katika kuhakikisha kwamba anaonyesha hisia zake za furaha mara baada ya Simba Sc kupigwa kipigo kizito cha magoli matatu kwa moja dhidi ya Singida Black Stars, Haji Manara amekuja na jina jipya la utani ambalo amewatungia watani zake wa jadi yaani Simba Sc.

Manara kupitia katika ukurasa wake wa Instagram amechapisha taarifa iliyobeba jina hilo ambalo ni “Manyigu Fc”,. Ikumbukwe kwamba Simba Sc na Yanga Sc wamekuwa na utamaduni wa kutungiana majina ya utani na yanayokera kwa lengo la kuendeleza utani wao wa jadi.

Mpaka sasa Manara amewai kuwatungia Simba Sc majina mawili ya utani ambayo ni Makolo Fc pamoja na Madunduka Fc na sasa ameamua kuongeza jina jipya ambalo ni Manyigu Fc kwa lenho la kuendelea kuwakera mashabiki na wadau wa klabu ya Simba Sc.

Ukiachana na majina haya ya utani kutoka kwa Manara kwenda Simba Sc, pia kuna majina ya utani ambayo Simba Sc huwa wanawatania Yanga Sc kama vile Utopolo Fc na Nyuma Mwiko Fc, yote haya yanafanyika kwa lengo kuu la kutaka kuendeleza dhana ya utani wa jadi uliopo baina ya timu hizi tangu enzi na enzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *