ASTON VILLA wameulizia kama wataweza kupata huduma ya mlinzi wa kushoto wa Goztepe Novatus Miroshi katika dirisha kubwa la usajili, uongozi wa Goztepe unafikiria kwa kina biashara hio licha ya Novatus kuwa na mkataba mpaka 2028 klabuni hapo.
Novatus Dismas alijiunga na klabu ya Goztepe ya Uturuki mnamo Julai 2024 kwa mkataba wa miaka minne, akitokea Zulte Waregem ya Ubelgiji.
Katika msimu wa 2024/2025, ameonyesha kiwango kizuri akiwa na Goztepe, akicheza mechi 19 na kufunga mabao 4 katika ligi ya Super Lig ya Uturuki.
Kwa kuwa bado ana mkataba unaoendelea hadi Juni 2028 itawalazimu Aston Villa kuvunja mkataba ili kuweza kupata huduma yake, inaelezwa kuwa makadirio [thamani] ya kuvunja mkataba wake ni € 3.7 Million hadi € 6.2 Million endapo Aston Villa watakubali kumnunua.
