Marry wa Mwijaku Aliyemzalilisha Mwenzake Akosa Dhamani
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mary Gervas Matogolo (22), amewekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana kufuatia kesi ya Jinai inayomkabili yeye na Wanafunzi wenzake wawili, wakidaiwa kumshambulia mwenzao kwa kumgombania Msanii na Mtangazaji wa Redio, Burton Mwemba maarufu Mwijaku
Mary na wenzake, Ryner Ponci Mkwawili wa Chuo Kikuu Ardhi na Asha Suleiman Juma wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), walisomewa mashtaka 8 yakiwemo kusababisha madhara ya Mwilini, kutishia kuua, kusambaza taarifa za uongo kupitia Mitandao ya Kijamii na Uharibifu wa Mali
Ryner na Asha walitimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana, Mary alishindwa kutimiza vigezo na hivyo kupelekwa mahabusu hadi Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena