
Oktoba 21 ya mwaka 2019 ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa GEORGE AMBANGILE kuhamia Wasafi Media nikiwa ” Football Analyst ” . Nilipokelewa vizuri , nikapewa platform ya kuonesha kipaji changu , nikakua zaidi .
Baada ya miaka takribani Saba , cycle yangu imefikia tamati ndani ya Wasafi Media . It was quite a journey na najivunia , nashukuru , na kuthamini kila dakika niliyotumikia Wasafi Media .
Naishukuru sana Kampuni , imenipa vitu vingi sana ,moyo wangu umejaa shukrani .
Kipekee kabisa namshukuru CEO @diamondplatnumz kwa thamani uliyonipa , i will never forget it . Asante sana Boss .
Bila kusahau nawashukuru wafanyakazi wenzangu wote ambao tumefanya kazi kwa pamoja Wasafi Media kuanzia kipindi cha michezo mpaka wa vipindi vingine na wafanyakazi wa idara tofauti , mchango wenu kwangu una thamani kubwa sana . God bless you all .
Wale wote ambao walinipa thamani ya muda wao , masikio yao kusikiliza kazi yangu Radioni , cha kuwalipa sina maana bila nyie ngumu kuwa na George Ambangile bora , nawashukuru sana tena sana . Ambangile hayupo tena Wasafi Media lakini naomba muendelee kuwa ” LOYAL ” kwa Wasafi Media . ASANTENI SANA
THANK YOU SO MUCH WASAFI MEDIA AND GOODBYE
” The World is Yours ”
GEORGE AMBANGIL
