
Mbappe Mbele ya Messi Ufungaji Magoli, Saka Apiga Hat Trick, England Mshindi wa Tatu Kombe la Dunia 2026
TIMU ya Taifa ya England imemaliza nafasi ya tatu ikitwaa medali ya shaba kama mshindi wa tatu wa Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 huku Ufaransa ikimaliza nafasi ya nne baada ya kipigo cha 6-4 kwenye mchezo huo.
Bukayo Saka amefunga magoli matatu ‘hat-trick’ wakati Jude Bellingham akifunga bao lake la saba kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 akiwa mfungaji bora wa England kwenye michuano hiyo bao moja mbele ya Harry Kane mwenye magoli sita.
Kylian Mbappe amefunga magoli mawili na kufikisha magoli 10 kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2026 huku akiwa mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya Kombe la Dunia akifikisha magoli 22, moja mbele ya Messi.
FT: France 🇫🇷 4-6 🏴 England
⚽ 48’ Mbappe
⚽ 66’ Mbappe
⚽ 54’ Barcola
⚽ 90+6’ Dembele
⚽ 03’ Rice
⚽ 18’ Konsa
⚽ 37’ Saka
⚽ 45+2’ Saka
⚽ 87’ saka
⚽ 90+8’ Bellingham
