MWIMBAJI Ibraah ameondoka muda huu kwenye ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) , huku akisema kuwa wamezungumzia migogoro iliyopo kati yake na Bosi wake Harmonize na kwamba mam-bo yameenda freshi tu, bila kufafanua kwa kina.
Ibraah amezungumza na waandishi wa habari muda huu mara baada ya kutoka ofisi za Basata alizoitwa yeye na Harmonize ili kujadili sakata lao linaloendelea na amesema anashukuru mambo yanaenda vi-zuri na kila kitu amewaachia uongozi wa BASATA watatoa majibu.
“Nashukuru Mungu mambo yanaenda vizuri, na sababu ya kuitwa ni kuzungumzia migogoro inayoen-delea, hivyo tumefanya mazungumzo na BASATA tumewaachia uongozi washughulikie wao watatoa majibu,” amesema Ibraah.
Kwa upande wa Mwanasheria wa Ibraah amesema, BASATA watakapotoa majibu juu ya kinachoen-delea Ibraah ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida.
“Kuhusu Ibraah kuendelea kufanya kazi kama kawaida, tunasubiri majibu ya BASATA ,baada ya hapo Ibraah ataendelea na yake,” amesema mwanasheria huyo wa Ibraah bila ya kutaja jina lake.
Ibraah na Harmonize wamekuwa wakilumbana mtandaoni, kutokana na msimamo wa mwimbaji huyo kutaka kujiondoa katika Lebo ya Konde Gang na kudai anatakiwa kulia Sh 1 Bilioni na mzozo huo uliufanya uongozi wa Basata kuwaita Jumatatu iliyopita, lakini mambo hayakuenda sawa na leo ime-waita tena na kumaliza kika muda mchache uliopita.