Sikukuuu ya EID El -Adh’haa Itakuwa Mei 27, 2026

Sikukuuu ya EID El -Adh'haa Itakuwa Mei 27, 2026
Sikukuuu ya EID El -Adh’haa Itakuwa Mei 27, 2026

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid Ei-Adh’haa itakuwa siku ya Jumatano tarehe 27/05/2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaj Nuhu Jabiri Mruma, imesema Sherehe za Eid Ei-Adh’ha kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam.

Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid mara tu baada ya Swala.

“Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mh. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dr. Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu hiyo” imesema taarifa hiyo.

Related Posts