
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Bara John Heche, amesema mwelekeo wa Chama hicho baada ya Mahakama ya Rufaa kuwaondolea zuio la kufanya Siasa ni kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, anaachiwa huru.
Heche ameeleza hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo April 15,2026, Heche amesema ““Mwelekeo wetu ni kuhakikisha Mwenyekiti wetu anaachiwa huru ndio tunaanza nalo, Mwenyekiti wetu sio Mhaini, mwelekeo wetu na Wanachama wetu ni kutaka Tundu Lissu atoke ndani mwaka mmoja ni mwingi sana, hapa duniani ni Mungu anatuweka ndiye anatupa siku za kuishi, Mtu mmoja akikanyaga hata lisaa limoja la kwako hawezi kukurudishia hilo lisaa achilia mbali siku”
“Hakuna hata mmoja kati ya wanaomshikilia Lissu ambaye anaweza kumrudishia mwaka wake mmoja ambaye amemfungia mule ndani, huo mwaka umepita kwa uharibifu kwa uongo, kampeni yetu Nchi nzima ni kutaka Lissu aachiwe mara moja awe huru tuanze shughuli yetu, hatuna jambo dogo”
“Leo ni siku ya furaha nimefurahi tuko hapa nilipamiss hapa ndani, Vyombo vya Habari nawaasa dunia ya sasa msipo cover ukweli, Mtu anaweza kukaa chumbani akajirekodi na Watu wakaona, tunashukuru mliokuja tutazungumza zaidi baada ya Kamati kuu ndio tutasema hatua gani tutachukua lakini hatupigi magoti, haturudi nyuma, hatumsujudii Binadamu tunasonga mbele kubadilisha Nchi hii”
