Klabu ya Geita Gold Yarejea Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara

πŽπ…π…πˆπ‚πˆπ€π‹: Klabu ya Geita Gold inayofundishwa na Kocha, Zubery Katwila imerejea Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Songea United katika uwanja wake wa nyumbani wa Nyamkumbu.

Geita Gold iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024 imepanda daraja baada ya kufikisha pointi 71 baada ya mechi 28 wakishinda mechi 22 sare 5 na kichapo kimoja ambapo pointi hizo haziwezi kufikiwa na Polisi Tanzania inayoshika nafasi ya tatu na pointi 60, kwani hata ikishinda mechi zote tatu itaishia 69.

Related Posts