
Klabu ya Singida BS imetozwa faini ya Tsh. milioni tano kwa kosa la viongozi wake wawili kuingia kiwanjani na kumwaga vimiminika, tukio lililotafsiriwa kama vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina kabla ya timu kutoka kwa ajili ya kupasha moto misuli kuelekea mchezo dhidi ya TRA United.
Adhabu hiyo imetolewa leo Aprili 20, 2026 na kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kikao chake cha Aprili 18, 2026 ambapo tukio hilo limetokea kuelekea mchezo huo uliomalizika kwa ushindi wa 2-0 kwa wenyeji TRA United katika dimba la Sheikh Amri Kaluta Abeid, Arusha.
