KOCHA wa zamani Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa miongoni mwa timu hatari zijazo katika Ligi Kuu Bara ni Singida Black Stars.
“Nilisema kuwa Singida itakuwa timu tishio na taratibu naona matunda ya maneno yangu,naamini hii itakuja kuwasumbua Simba na Yanga. Wengi wamezoea kuona timu mbili tu zikiwa kwenye ushindani,wanasahau Singida inasogea kwa kasi na ghafla wataiona juu sana,” alisema na kuongeza:
“Imefanya usajili mkubwa sana ambao kimataifa unaweza kuwapa matokeo makubwa ambayo yatawashangaza wengi.
Niwapongeze sana msimu ujao najua watakaza zaidi kamba zao ili wasiishie nafasi ya tano bora wafike juu zaidi.”
Ikumbukwe kuwa,Singida Black Stars imeitoa Simba katika michuano ya Shirikisho katika hatua ya Nusu Fainali kwa kuichapa mabao 3-1. Huku katika ligi ikimaliza na moto wa kushika nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 28, ikishinda 16, ikipoteza saba na sare tano,i kifikisha pointi 53.