
Manchester City imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Carabao baada ya kuichapa Brighton & Hove Albion kwa penalti 4-3 katika uwanja wa Etihad, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Timu zingine zilizofuzu robo fainali ni Fleetwood Town iliyowatoa Arsenal kwa penalti 5-3), Bradford City iliyoitoa Peterborough United Kwa ushindi wa 2-0, AFC Bournemouth iliyoichapa Aston Villa 3-0, Crystal Palace iliyoiondosha Fulham kufuatia ushindi wa 1-0 na Sunderland iliyotinga hatua hiyo baada ya kuwatoa Brentford kwa ushindi wa 3-2.
Nafasi mbili za mwisho za nane bora zinatarajiwa kujazwa na washindi wa michezo kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea, pamoja na Everton dhidi ya Newcastle United.
FT: Man City 2-2 Brighton (P 4-3)
⚽ 40’ Kovacic
⚽ 72’ Vitor Reis
⚽ 30’ Yalcouye
⚽ 47’ Rutter
