Enzo PittauEnzo Pittau

Mwanasoka wa Argentina Enzo Pittau amefariki Dunia baada ya kuanguka Uwanjani dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza cha mchezo kwa mshtuko wa Moyo.

Kabla ya hayo yote kutokea, alitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kusema kwamba alikuwa amejitolea kila kitu kwa mchezo huu.

Baada ya kifo hiki cha ghafla, mechi iliahirishwa mara moja na usimamizi wa timu ya Don Orione ulionyesha mshikamano wake na mchezaji huyo.

Vyombo vya habari vya eneo hilo vinasema Pittau alikuwa amerejea Chaco ili kuwa karibu na familia yake baada ya babu yake kuwa na matatizo ya kiafya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *