Msukuma: Askofu Gwajima Anaponzwa na Presha ya Jimbo

Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Kasheku “Musukuma”, amesimama bungeni na kumkosoa vikali Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima @bishopgwajima kutokana na kauli zake kwenye mkutano na waandishi wa habari, akidai kuwa ni kuingilia mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan

Akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Musukuma amesema ni vyema wabunge na viongozi wa kisiasa wakamuachia Rais nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba.

Amesema si sawa kwa viongozi kutumia majukwaa ya kisiasa na ya waandishi wa habari kuingilia maamuzi ya Rais, hasa katika uteuzi na mabadiliko ya nafasi za uongozi serikalini.

“tusilete presha za majimbo tukaanza kuingilia mamlaka, Rais ana nafasi ya kumtengua yeyote na kumuweka mtu yeyote, tusitumia upole wa Mama Samia kuanza kuingilia mpaka ‘state’ kupanga na kupangua, hapana! wananchi wetu wanatushangaa”, ameongeza Musukuma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *