Mudathir Yahya Afungiwa Michezo Mitatu, Kuikosa Simba Mei 3

Kiungo wa Yanga SC, Mudathir Yahya amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Tsh. milioni moja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji, Ibrahim Abraham wakati mchezo unaendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Aprili 18, 2026 baada ya kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi ambapo tukio hilo lilitokea kwenye mchezo wa Ligi kuu baina ya timu hizo uliomalizika kwa Yanga SC kushinda 3-0 katika dimba la CCM Kirumba, Mwanza.

Related Posts