PacomePacome

Pacome Zouzoua ni Kiungo Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kufikiri Uwanjani

JKT Tanzania imekwama katika mbio za kusaka tiketi ya michuano ya CAF baada ya kufungwa mabao 2-0 na Yanga SC katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), huku beki Wilson Nangu akisema kumkaba Pacome Zouzoua inahitaji umakini mkubwa.

Beki huyo chipukizi ameliambia Mwanaspoti kuwa
kiungo mshambuliaji huyo wa Yanga SC ni mchezaji mwenye kasi na akili ya kubadilisha mechi, jambo ambalo kwa beki yeyote anayemkaba anapaswa kufanya kazi ya ziada uwanjani.

Pacome amefunga mabao tisa na asisti tisa katika Ligi Kuu, jambo ambalo Nangu mwenye mabao mawili amedai katika mechi walizocheza dhidi ya Yanga SC msimu huu amegundua.

Wilson Nangu 🗣.”Ni kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kufikiria nyakati awapo uwanjani, mfano mipira ya kufa ambayo beki anaweza akaidharau. Unaweza ukashtukia Pacome kashaufikia mpira na unaweza ukaleta madhara langoni.”

Credit × Mwanaspoti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *