Profesa Mkenda: Mtoto wa waziri kupata mkopo wa elimu ni wizi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amesema mtoto wa waziri au katibu mkuu wa wizara kupata mkopo unaotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ni wizi kwakua kitendo hicho kinawanyima fursa wanaostahili.
Prof. Mkenda, amesema hayo leo Mei 27, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara yake kwa ipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
“Mtoto wa waziri au katibu mkuu kupata mkopo huu unaotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu ni wizi kwani hali hiyo inawanyima haki wenye uhitaji, mimi mwenyewe kabla sijawa waziri nilisomesha hakupatiwa mkopo,”amesema
Aidha, amesema serikali bado inafanyia kazi mfumo wa utoaji wa mikopo hiyo ili wanaopata wawe tuu ni wale wanaostahili bila kumpendelea ama kumnyima fursa hiyo mtu anayestahili kupata.