Rage Amkingia Kifua Mangungu, Aikosoa Bodi ya Simba SC

Rage Amkingia Kifua Mangungu, Aikosoa Bodi ya Simba SC
Rage Amkingia Kifua Mangungu, Aikosoa Bodi ya Simba SC

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amekosoa vikali hatua ya Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kuitisha Mkutano Mkuu wa Kawaida na Uchaguzi bila kumhusisha Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu.

Katika tamko lake kupitia chombo cha habari cha TV3 Tanzania, Rage amesisitiza kuwa hatua hiyo inakiuka Katiba ya Simba, kwani Bodi haina mamlaka ya kisheria ya kusimama pekee na kuitisha mkutano huo na kubainisha kuwa kikatiba, Mwenyekiti aliyechaguliwa na wanachama ndiye mwenye mamlaka hayo baada ya kushauriana na Bodi, akikaririwa kusema, “Bodi haiwezi kumwalika Mwenyekiti, Mwenyekiti ndiye anayeialika Bodi.”

Kufuatia msuguano huo, Rage ametangaza kumuunga mkono kwa asilimia mia moja Mwenyekiti wa sasa, Murtaza Mangungu, katika msimamo wake wa kupinga mchakato huo na kuitisha vikao vya dharura huku akiaamini kuwa uamuzi wa Bodi wa kutoa matangazo ya mikutano na uchaguzi yenyewe, badala ya kushauriana na Mwenyekiti, unazua taharuki na migogoro isiyo ya lazima miongoni mwa wanachama wa klabu hiyo.

Aidha Rage ametoa wito wa kulinda nguvu na sauti ya wanachama, akionya kuwa mfumo wa sasa unampa mwekezaji mamlaka makubwa kupitia Bodi huku viongozi wa wanachama wakiachwa kama wasindikizaji akiwataka viongozi kusimamia misingi ya katiba ili kuhakikisha upande wa wanachama, ambao ndio wamiliki halisi wa klabu, unabaki na kauli na nguvu thabiti ya kimaamuzi.

Related Posts