Robert Pattinson Atangazwa Kuwa James Bond Mpya, Denis Villeneuve Kuongoza Filamu Ijayo

Robert Pattinson Atangazwa Kuwa James Bond Mpya, Denis Villeneuve Kuongoza Filamu Ijayo
Robert Pattinson Atangazwa Kuwa James Bond Mpya 

Robert Pattinson Atangazwa Kuwa James Bond Mpya, Denis Villeneuve Kuongoza Filamu Ijayo

Los Angeles, Marekani – Muigizaji nyota wa Hollywood, Robert Pattinson, aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu maarufu kama The Batman na Twilight, ametangazwa kuwa ndiye atakayekuwa mhusika mkuu mpya wa filamu za James Bond.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka tasnia ya filamu, Pattinson anachukua mikoba ya jasusi maarufu wa Uingereza, Agent 007, nafasi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikichezwa na muigizaji Daniel Craig.

Mabadiliko Makubwa Kwenye Uzalishaji

Mbali na uteuzi wa Pattinson kama sura mpya ya 007, taarifa hizo zinaeleza kuwa muongozaji mahiri wa filamu za Dune, Denis Villeneuve, ametajwa kuwa ndiye atakayeongoza (direct) filamu hiyo inayofuata ya James Bond, hatua inayotazamiwa kuleta mwelekeo mpya na wa kisasa katika mfululizo wa filamu hizo.

Kauli ya Robert Pattinson

Akizungumzia uteuzi huo wenye hadhi ya juu katika tasnia ya sinema duniani, Robert Pattinson ameeleza furaha yake akibainisha kuwa kuvaa uhusika wa James Bond ni hatua kubwa katika safari yake ya sanaa.

“Kupata nafasi ya kuigiza kama James Bond ni ndoto iliyotimia na heshima kubwa sana katika maisha yangu ya uigizaji,” amenukuliwa akisema Pattinson.

Uteuzi huu unatarajiwa kuamsha shauku mpya miongoni mwa mashabiki wa filamu duniani kote ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu kujua ni nani angechukua nafasi hiyo tangu Daniel Craig alipoachana na uhusika huo.

Related Posts