
Ruby Aamua Kuacha Muziki wa Bongo Fleva na Kumrudia Yesu
Mwanamuziki mashuhuri nchini Tanzania, Ruby, ametangaza kuanza sura mpya ya maisha yake kwa kuamua kuacha muziki wa Bongo Fleva na kuwekeza maisha yake katika kumtumikia Mungu.
Akiwa mmoja wa waimbaji wa kike walioacha alama kubwa nchini kupitia sauti yake ya pekee na uwezo wa kutumbuiza jukwaani (LIVE show), Ruby amekuwa akionyesha mabadiliko ya kiroho kwa muda sasa. Kupitia kauli na maisha yake ya hivi karibuni, msanii huyo ameweka wazi uamuzi wake wa kuingia kwenye huduma na kumfuata Yesu Kristo.
Uamuzi huo unagonga fikra za mashabiki wengi waliomfuatilia kwa miaka mingi, huku wengi wakimtakia kheri katika safari yake mpya ya kiroho licha ya kwamba sauti yake na nyimbo zake zitaendelea kukumbukwa kwenye tasnia ya burudani.
