
Mwanamitindo na staa maarufu wa mitandao ya kijamii, Nana Dollz, amewakosha mashabiki wake baada ya kushusha ujumbe mzito unaosisitiza umuhimu wa kujikubali na kusimama kwenye utofauti wako bila kuiga wengine.
Kupitia ukurasa wake, Nana Dollz ameweka wazi msimamo wake wa maisha kwa kuandika: “I Was Born To Stand Out Not To Fit In✨🐝” (Akimaanisha: ‘Nilizaliwa ili niwe wa kipekee na nionekane, na siyo kujifanya ninafanana na kila mtu’).
Ujumbe huo umepokelewa kwa hisia chanya na wafuasi wake wengi mtandaoni, ambao wamempongeza kwa kuwapa motisha ya kujiamini na kutovunjwa moyo na maneno au shinikizo la jamii. Nana Dollz anaendelea kushikilia nafasi yake kama mmoja wa mastaa wa kike wanaofuatiliwa zaidi mtandaoni kutokana na mtindo wake wa maisha na jumbe zake za kujenga
