Simba Alisononesha Taifa, RS Berkane Bingwa Kombe la Shirikisho Afrika
RS Berkane imetwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa mara ya tatu kihistoria kufuatia ushindi wa jumla wa 3-1 dhidi ya Simba Sc katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Simba Sc imepoteza fainali nyingine tena mbele ya Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kama ilivyokuwa mwaka 1993 ilipopoteza fainali nyingine mbele ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi, baba yake ya Dkt. Mwinyi.
FT: Simba Sc 🇹🇿 1-1 🇲🇦 RS Berkane (Agg 1-3)
âš½ 17′ Mutale
🟥 50′ Kagoma
âš½ 90+3′ Sidibe