Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Gyokeres atishia kugoma ili kuondoka Sporting
Mshambuliaji wa Sporting anayewaniwa na Arsenal na Manchester United Viktor Gyokeres, 27, amekataa kufanya mazungumzo ya wazi na kutishia kugoma huku akishinikiza kuondoka kwa klabu hiyo ya Ureno. (Mirror)
Fulham imekataa ofa ya pauni milioni 26, pamoja na nyongeza ya pauni milioni 6, kutoka kwa Leeds iliyopanda daraja kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Rodrigo Muniz, 24. (Standard)
Lakini Fulham wenyewe inafikiria kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Marekani Ricardo Pepi, 22, ambaye anafuatiliwa na klabu kadhaa za Uhispania na Italia. (Fabrizio Romano)
Beki wa Arsenal Myles Lewis-Skelly anakaribia kusaini mkataba mpya ambao utamfanya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18 kuwa miongoni mwa wachezaji chipukizi wanaolipwa donge nono zaidi duniani. (Athletic – michango inahitajika)
Lakini meneja msaidizi Carlos Cuesta anatazamiwa kuondoka Arsenal ili kuchukua nafasi yake ya kwanza ya ukocha mkuu katika klabu ya Parma inayoshiriki ligi kuu ya Serie A. (Guardian)
Liverpool iko tayari kuvunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza kumsajili mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 25, msimu huu wa kiangazi. (Give Me Sport)
Maelezo ya picha,Beki wa Arsenal Myles Lewis-Skelly anakaribia kusaini mkataba mpya
Aston Villa iko tayari kumuuza kiungo wa kati Emi Buendia mwenye umri wa miaka 28 iwapo itapokea ofa ya zaidi ya £20m kwa Muargentina huyo. (Caught Offside)
Chelsea imefanya mawasiliano ya awali na Brighton kuhusu mshambuliaji wa Brazil Joao Pedro, 23, ambaye pia anasakwa na Newcastle. (Fabrizio Romano)
Brentford imeweka bei ya pauni milioni 50 kwa mshambuliaji Yoane Wissa, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo akinyatiwa na Nottingham Forest, Tottenham, Arsenal, Fenerbahce na Galatasaray. (Team Talk)
Mshambuliaji wa Nice na Ivory Coast Evann Guessand, 23, anavutia klabu za Leeds na Tottenham, ambazo zimewasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo. (TBR Football)
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.