Kijana Aliyerekodi Video ya Ajali ya Air India Ambayo Ilisambaa Mitandaoni
Kuangalia ndege lilikuwa jambo la kawaida kwake, baba yake Maganbhai Asari alisema.
Aryan alipenda sauti ya mngurumo ya injini iliyojaa hewani na kisha ikaongezeka zaidi ndege ilipokuwa ikipita juu yake, ikiacha nyuma nyuzi za chaki angani.
Alhamisi iliyopita, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alikuwa kwenye mtaro wa nyumba ya Bw Asari katika jiji la Ahmedabad, akitengeneza video za ndege, wakati ndege ya Air India Dreamliner 787-8 ilipoanguka mbele ya macho yake na kuwaka moto, na kuwaua 241 waliokuwa ndani. Takribani watu 30 pia walipoteza maisha ardhini.
“Niliiona ndege. Ilikuwa ikishuka na kushuka. Kisha ikayumba na kuanguka mbele ya macho yangu,” aliiambia BBC Gujarati katika mahojiano mapema wiki hii.
Video hiyo, ambayo sasa ni kidokezo muhimu kwa wachunguzi wanaojaribu kutafuta chanzo cha ajali hiyo, imezua gumzo kupitia vyombo vya habari na kumweka Aryan , mwanafunzi wa shule ya sekondari katikati ya moja ya majanga mabaya zaidi ya anga katika historia ya nchi.
“Tumejawa na maombi ya mahojiano. Wanahabari wamekuwa wakizunguka nyumba yangu usiku na mchana wakiomba kuzungumza naye,” Bw Asari aliambia BBC.
Tukio hilo na lililofuata tangu wakati huo, limekuwa na “athari mbaya” kwa Aryan, ambaye ameumizwa na kile alichokiona. “Mwanangu anaogopa sana hadi ameacha kutumia simu yake,” Bw Asari alisema.
Askari mstaafu wa jeshi, ambaye sasa anafanya kazi na huduma ya metro ya jiji, Bw Asari amekuwa akikaa kwa miaka mitatu katika mtaa ulio karibu na uwanja wa ndege.
Mkewe na watoto wawili , Aryan na dada yake mkubwa, wanaishi katika kijiji cha mababu zao karibu na mpaka kati ya majimbo ya Gujarat na Rajasthan.
“Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Aryan kufika Ahmedabad. Kwa kweli, ilikuwa mara ya kwanza maishani mwake kuondoka kijijini,” Bw Asari alisema.
“Kila mara nilipiga simu, Aryan alikuwa akiuliza kama ninaweza kuona ndege kutoka kwenye ngazi zetu na ningemwambia unaweza kuona mamia ya ndege ya zikiruka angani.”
Aryan, alieleza, alikuwa mpenda ndege na alipenda kutazama zilipokuwa zikiruka angani juu ya kijiji chake. Wazo la kwamba angeweza kuwaona kwa ukaribu zaidi kutoka kwenye nyumba mpya ya baba yake lilimvutia sana.
Ndege hiyo ilipoteza mwelekeo na kuanguka katika eneo la makazi la jiji linaloitwa Meghaninagar
“Alisikika akiwa na hofu sana, ‘Niliiona baba, niliiona ikianguka,’ aliniambia na kuendelea kuniuliza nini kitampata. Nilimwambia atulie, asiwe na wasiwasi,” Bw Asari alisema. “Lakini alikuwa mwenye hofu.”
Bw Asari pia alimtaka mwanawe kutosambaza video hiyo zaidi. Hatahivyo, kwa kuogopa na kushtuka sana, Aryan aliituma kwa marafiki zake wachache. “Jambo lililofuata tulibaini, video ilikuwa kila mahali.”
Siku chache zilizofuata zilikuwa ndoto kwa familia.
Majirani, waandishi wa habari na watu wa kamera walifurika katika nyumba ndogo ya Bw Asari mchana na usiku, wakiomba kuzungumza na Aryan. “Hatukuweza kufanya lolote kuwazuia,” alisema.
Familia hiyo pia ilitembelewa na polisi, ambao walimpeleka Aryan kituoni na kurekodi taarifa yake.
Bw.Asari alifafanua, kwamba kinyume na ripoti, Aryan hakuzuiliwa, lakini polisi walimhoji kwa saa chache kuhusu kile alichokiona.
“Mwanangu alichanganyikiwa sana wakati huo tukaamua kumrudisha kijijini.”
Akiwa nyumbani, Aryan amerejea shuleni lakini “bado hajisikii vyema. Mama yake ananiambia kwamba kila mara simu yake inapolia, anaogopa”, Bw Asari alisema.
“Najua atakuwa sawa kwa wakati. Lakini sidhani mwanangu atajaribu kuitafuta ndege angani tena,” aliongeza.
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.