AZAM SAJILI ZAO KWA ASILIMIA KUBWA ZIMEFELI.
πMwisho wa msimu uliopita hata kabla dirisha kubwa la usajili halijafunguliwa Azam walianza kufanya sajili kwenye klabu yao hasa za wachezaji wa kimataifa na kwa Azam walianza na wachezaji raia wa Colombia wengi walikuwa na matumaini na sajili hizo.
πHata wakati wa dirisha kubwa bado viongozi wa Azam walikuwa bize sana kufanya sajili kwani walikuwa wawakilishi wa nchi kwenye CAF Champions league hivyo walikuwa kwenye wakati wa kujenga timu ya ushindani.
πSajili zilikuwa nyingi na karibia kila position walisajili kitu ambacho matarajio yalikuwa mengi kwa Azam msimu huu,Kwanza wengi walidhani watafanya vizuri CAF Champions league na hata kwenye ligi lakini yote yameenda tofauti.
πCAF Champions league hatua za awali tu waliondoshwa kwenye ligi kuu napo mambo yameshakuwa magumu kutoka kumaliza top two msimu uliopita hadi kuanza kuipambania top four msimu huu kitu ambacho ni big disappointed kwa fans wa Azam Fc.
πKwenye kombe la CRDB federation Cup napo wameondoshwa mapema licha ya misimu kadhaa kucheza fainali na nusu fainali ila awamu hii kwao imekuwa ngumu baada ya kutolewa na Mbeya city.
πHakuna mchezaji ambaye amekuwa surprise pale Azam kwa sajili zilizofanywa msimu huu ni yuleyule FEISAL SALUM ambaye bado ndio anabaki kuwa most valuable player kwenye kikosi cha Azam kutoka na ubora wake na consistency yake kwenye kikosi cha Azam
By Hansrafael

