Wananchi Wafurika Barabarani Iran Kuaga Mwili wa Khamenei

Wananchi Wafurika Barabarani Iran Kuaga Mwili wa Khamenei
Wananchi Wafurika Barabarani Iran Kuaga Mwili wa Khamenei

Mamilioni ya raia wa Iran wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wa Tehran kwa ajili ya mazishi ya Kiongozi Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Ali Khamenei, aliyefariki Februari 28 mwaka huu katika mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani msururu wa waombolezaji ulianza asubuhi na ulidumu kati ya saa 10 hadi 12, ukifuata njia ya kilomita 10 kupitia mitaa mikuu ya Tehran ikiwemo Damavand Street, Imam Hossein Square, Enqelab Street, Enqelab Square, na Azadi Square.

Mamlaka nchini Iran imetangaza kuwa mazishi hayo ni miongoni mwa tukio kubwa zaidi la umma katika historia ya kisasa ya nchi hiyo, huku makadirio yakionyesha kuwa kati ya watu milioni 10 hadi 20 walishiriki katika ibada hiyo.

Imeelezwa kuwa msururu huo wa mazishi ulionekana kujaa ishara za kisiasa, huku bendera nyekundu zilizoashiria kisasi zikitawala katika umati wa waombolezaji uliojitokeza kumuaga mpendwa wao.

Waombolezaji Iran
Pia imeelezwa kuwa waombolezaji walionekana wakiwa na mabango dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump, huku wengine wakirusha mawe kwenye picha yake kubwa katika ibada inayofanana na ibada ya “Kupiga mawe Ibilisi” wakati wa Hijja.
Katika hatua hiyo, picha mnato na mjongeo zilizochapishwa katika mitandao mbalimbali zimeonesha mabango makubwa yaliyoandikwa “We Will Kill Trump” yakionekana kwenye msururu huo wa waombolezaji.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa viongozi mbalimbali nao walishiriki katika mazishi hayo akiwemo Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf ambaye pia ni mjumbe mkuu wa mazungumzo na Marekani, na Kamanda wa Kikosi cha Quds Esmail Qaani.

Pia ilielezwa kuwa Rais wa zamani Mahmoud Ahmadinejad, ambaye alikuwa ametoweka hadharani tangu kuanza kwa vita Februari 28 na kulikuwa na uvumi kwamba aliuawa, alionekana kwenye msururu wa mazishi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana hadharani tangu kuanza kwa vita.

Related Posts