Watu1,609,078 Wanatumia ARV za Kufubaza Virusi vya Ukimwi Tanzania

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, (@mohamed_mchengerwa ) amesema Watu 1,609,078 kati ya waliopima na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI, hii ikiwa ni sawa na asilimia 94.7 (95 ya pili).

Akiongea leo May 11,2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2026/2027, Mchengerwa amesema “Aidha, jumla ya WAVIU 1,343,112 wanaotumia dawa za ARV walifanya vipimo vya kujua wingi wa Virusi vya UKIMWI, ambapo WAVIU 1,317,593 sawa na asilimia 98.1 walifubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (95 ya tatu)”

Related Posts