
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema limepokea taarifa ya kifo cha mtu ambaye tarehe 11 Mei, 2026 saa 04:30 Asubuhi mwili wake ulikutwa kwenye maji eneo la daraja la Salender llala na mwili huo ambao haukuwa na jeraha lolote.
Taarifa ya leo Mei 11, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro imeeleza kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa wa mwili huo ni wa mtu aitwaye Aisha Miraji mkazi wa Nzasa Temeke ambaye aliwapotea wazazi wake eneo la Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mnamo tarehe 10 Mei, 2026 wakati mtu huyo akiwa na wazazi wake anapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili kwa maradhi ambayo kwa muda tofauti tofauti katika miaka mitano yalikuwa yanamsumbua, aliwapotea akiwa eneo hilo la Muhimbili mpaka mwili wake ulipokutwa tarehe na eneo lililotajwa hapo juu.
Taarifa ya SACP Jumanne Muliro imesema wazazi wa marehemu wamezielezea changamoto za kiafya za mtoto wao alizokuwa anazipitia lakini hata hivyo Polisi wanachunguza taarifa hiyo.
