Yanga Yataja Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Kama Lengo Kuu Msimu Huu

Uongozi wa Young Africans (Yanga SC) umehitimisha uvumi na kuweka wazi kuwa shabaha yao kuu katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ni kufika angalau hatua ya robo fainali. Akizungumza akiwa jijini Gaborone, Botswana, Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Hajji, ameeleza kuwa klabu hiyo imejipanga vyema kwa kuboresha benchi la ufundi na kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa michuano ya CAF ili kufikia malengo hayo.

Arafat amewataka Watanzania wanaoishi Botswana na Afrika Kusini kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti Yanga kwenye mchezo wao dhidi ya Gaborone United. Mbali na mchezo huo, klabu pia inatarajia kuzindua tawi jipya la mashabiki jijini Gaborone ili kuendelea kukuza chapa ya Yanga kimataifa.

Related Posts