Kamati ya Ndani ya Maandalizi ya AFCON nchini Kenya imesema itaunga mkono kuahirishwa kwa michuano ya AFCON 2027 hadi mwaka 2028, kutokana na uwezekano wa vurugu zinazoweza kuhusiana na uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 2027.
Timu ya ukaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa sasa ipo Tanzania na inatarajia kufanya kikao kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
