
Zaidi ya Mashabiki Milioni 30 wa Real Madrid wamesaini ombi la kumtaka Kylian Mbappé aondoke katika klabu hiyo kutokana na kukosa matokeo na kutofanya vizuri nje ya Uwanja.
Siku mbili zilizopita, ombi lilizinduliwa kwa Mashabiki wa Real Madrid kusaini ombi la kutaka Kylian Mbappé aondoke katika klabu hiyo.
Ombi hilo awali liliwekwa kwa lengo la saini 200, lakini kwa siku moja tu, saini Milioni 18 zilikusanywa, na ndani ya saa 48, saini Milioni 30 zilipatikana.
Mchezaji huyo anatuhumiwa na Wachezaji wenzake kuwa ni msaliti jambo ambalo linaleta mgawanyiko miongoni mwa wachezaji wa Real Madrid hasa kikosini.
Mbappe, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Uhispania Juni 2024 akitokea Paris Saint-Germain, alitia saini Mkataba utakaomweka hadi 2029.
