Kaizer Chiefs Yaitolea Macho Saini ya Prince Dube wa Yanga SC

Kaizer Chiefs Yaitolea Macho Saini ya Prince Dube wa Yanga SC
Kaizer Chiefs Yaitolea Macho Saini ya Prince Dube wa Yanga SC

Klabu maarufu ya Afrika Kusini, Kaizer Chiefs, imeonyesha nia thabiti ya kutaka saini ya mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Kaizer Chiefs wamejipanga vizuri kifedha na wameweka mezani “pesa ndefu” ili kumshawishi mchezaji huyo raia wa Zimbabwe kujiunga nao.

Pamoja na ofa hiyo kubwa, mabingwa wa soka nchini Yanga SC, bado wanasemekana kuhitaji huduma ya Dube na hawajajipanga kuachana naye kirahisi, jambo linalofanya usajili huu kuwa wa vuta nikuvute.

Related Posts