
Rais Samia Suluhu Hassan, amemjulia hali mchezaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, kufuatia majeraha aliyopata katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam hivi karibuni.
Pacome Zouzoua anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Rais Samia alifika hospitalini hapo leo Julai 6, 2026 kumjulia hali Sheikh Rashid Hamad Othman, kaka mkubwa wa Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, anayepatiwa matibabu hospitalini hapo.
Akiwa hospitalini hapo, Rais Samia alielezwa uwepo wa Pacome ndipo akatumia fursa hiyo kumtembelea na kumpa pole kutokana na majeraha yake.
