
Timu ya Taifa ya Uhispania imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa mara ya pili kihistoria kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya waliokuwa Mabingwa watetezi, Argentina katika dimba la New York New Jersey, Marekani kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2026.
Bao pekee la Ferran Torres limetosha kuwavua Argentina ubingwa wa Dunia Lionel Messi akikosa fursa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya kuiongoza timu kubeba ubingwa wa Dunia mwaka 2022.
Kylian Mbappe amemaliza kama mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 akifunga mabao 10, mawili mbele ya Lionel Messi mwenye magoli 8.
FT: Argentina 🇦🇷 0-1 🇪🇸 Spain
🟥 90+3’ Enzo
⚽ 106’ Torres
