Usajili wa Peter Shalulile Yanga SC: Ujumbe Mzito kwa Soka la Afrika na Mapinduzi ya Ligi Kuu ya Tanzania

Transfer ya mshambuliaji hatari raia wa Namibia, Peter Shalulile, kujiunga na Yanga SC imekuwa gumzo kubwa sio tu Tanzania na Namibia, bali katika mataifa ya Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla.

Huu si usajili wa kawaida au wa bahati mbaya; ni matokeo ya kazi kubwa na ya kitaalamu iliyofanywa na uongozi wa Yanga SC. Pesa pekee isingeweza kumng’oa Shalulile—mfungaji wa muda wote wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) mwenye zaidi ya mabao 100. Kilichofanya dili hili likamilike ni mpango mkakati (project) uliomshawishi mchezaji wa kiwango chake.

Kukua kwa Mpira wa Tanzania
Miaka 10 iliyopita, mpinzani mkuu wa klabu zetu alikuwa APR, Kiyovu, Gor Mahia au Tusker, huku michuano ya CECAFA Kagame Cup ikionekana kama ‘Kombe la Dunia’ letu. Leo hii, pengo limekuwa kubwa mno. Viongozi wa soka wa sasa nchini, wakiongozwa na watu kama Injinia Hersi Said (@caamil_88), wameleta mapinduzi makubwa mezani. Wamevunja minyororo na makufuli ya zamani ambapo timu zetu zilikuwa zikitumiwa tu na wachezaji wakubwa kupandisha thamani zao kabla ya kukimbilia klabu zingine.

Athari kwa Ligi Kuu ya NBC
Kama vile usajili wa Cristiano Ronaldo ulivyobadilisha taswira ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia, ujio wa Peter Shalulile nchini Tanzania ni Statement Signing. Usajili huu si faida kwa Yanga pekee, bali ni ushindi kwa Ligi Kuu ya NBC kwani utavuta macho ya wadau wengi zaidi wa soka barani Afrika.

Related Posts