
Klabu ya Simba imepoteza mchezo wake wa pili mfululizo wa kirafiki huko Afrika Kusini walipoweka kambi ya siku 10 baada ya kukubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Sekhukhune United kwenye mchezo wao wa pili wa kirafiki ambao unahitimisha kambi hiyo.
Kipigo hicho kinakuja siku moja baada ya kipigo cha 1-0 dhidi ya Polokwane City ya Nchini Afrika Kusini jana ikiwa NI muendelezo wa maandalizi ya mechi zake zijazo ukiwemo mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa Oktoba 10.
FT: Sekhukhune United 2-1 Simba SC
