Nature

Haji Manara Ashinda Kura za Maoni Udiwani Kariakoo

Kada wa CCM na Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV, Haji Sunday Manara, ameshinda katika kura za maoni za kuwania nafasi ya udiwani katika Kata ya Kariakoo, Jijini Dar es salaam akiwashinda Wagombea wenzake wanne.

Wakitangaza matokeo leo August 04,2025 Wasimamizi wa uchaguzi wamesema Haji Manara amepata kura 136, Daudi Simba kura 85, Abdul Masamaki (Diwani anayemaliza muda wake) kura 31 na Siza Mazongela kura 0.

Kwa ushindi huo, Manara ameongoza kwa tofauti ya kura 51 dhidi ya Mpinzani wake wa karibu, Daudi Simba.

Related Posts