Stephen WasiraStephen Wasira

Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla amesema kutoonekana kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Stephen Wasira ni suala la ratiba na si vinginevyo kama inavyoelezwa.

Makalla amebainisha hilo kufuatia kauli mbalimbali zinazoibuliwa katika mitandao ya kijamii kutoka kwa baadhi ya wadau wakihoji alipo Mhe. Wasira ambaye hakuonekana kwa siku kadhaa hadharani.

Makalla amejibu swali hilo leo, Jumamosi Mei 17, 2025 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu Mei 29 na 30, 2025.

Amesema ni kawaida kwa kiongozi kupumzika baada ya ziara na shughuli mbalimbali za kiofisi kama ambavyo mwingine yeyote angefanya.

“Ni Mzee hana jambo lolote kwa hiyo ni ratiba kwamba bwana nitafanya hapa, nikikamilisha nitapumzika kuna jambo la familia, kuona watoto, hata mimi mwenyewe lazima nijiwekee hilo,” amesema Makalla.

Akifafanua zaidi, amesema hata yeye amekuwa akipumzika baada ya ziara, anafanya kazi nyingine za kiofisi na vikao vya kawaida.

“Kwa hiyo hata mimi nikipotea wiki moja mtasema mwenezi amekata moto au amekata pumzi hapana bwana ni suala la ratiba,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *