Mchungaji Maarufu Nchini Nigeria Awaomba Msamaha Mashabiki wa Arsenal Baada ya Utabiri wa Uongo

Mchungaji Maarufu Nchini Nigeria Awaomba Msamaha Mashabiki wa Arsenal Baada ya Utabiri wa Uongo
Mchungaji Maarufu Nchini Nigeria Awaomba Msamaha Mashabiki wa Arsenal Baada ya Utabiri wa Uongo

Mchungaji maarufu nchini Nigeria, Dolapo Lawal, ameomba radhi kwa Mashabiki wa Arsenal F.C. baada ya kutoa utabiri ambao wengi wameuita Unabii ulioshindwa kuhusu nafasi ya Klabu hiyo kushinda taji la Ligi kuu England.

Lawal alikuwa ametabiri kuwa Arsenal haitakuwa Mabingwa wa Premier League msimu huu, jambo lililozua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya timu hiyo kutwaa Ubingwa.

Katika ujumbe wake wa kuomba radhi, Mchungaji huyo alisema hakukusudia kuwapa Mashabiki matumaini ya uongo, huku akisisitiza kuwa yeye ni binadamu ambaye anaweza kukosea.

Kauli yake imeendelea kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, ambapo baadhi ya Mashabiki walimkejeli huku wengine wakisema kuwa alifanya vizuri kwa kuomba msamaha.

Related Posts