Baada ya Tunisia Kumfurumusha Kocha Baada ya Kipigo cha Bao Tano, Kocha Mpya Huyu

Kocha raia wa Ufaransa, HervΓ© Renard
Kocha raia wa Ufaransa, HervΓ© Renard

Kocha raia wa Ufaransa, HervΓ© Renard, ameteuliwa kuwa Kocha Mpya wa timu ya Taifa ya Tunisia, kwa ajili ya kampeni ya kombe la Dunia 2026.

Uamuzi huo unakuja baada ya Shirikisho la soka la Tunisia kumtimua aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sabri Lamouchi, kufuatia kipigo kizito cha mabao 5-1 kutoka kwa Sweden katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia 2026.

Rais wa Shirikisho la soka la Tunisia, Moez Nasri, alitangaza kupitia Televisheni ya taifa kuwa Renard ndiye atakayechukua nafasi ya Lamouchi na kuiongoza Tunisia katika mechi zilizobaki za Mashindano hayo.

Hii itakuwa mara ya tatu kwa HervΓ© Renard kushiriki Kombe la Dunia akiwa Kocha, baada ya kuongoza timu mbalimbali katika michuano hiyo. Tunisia inatumaini uzoefu wake mkubwa utaisaidia kurejea katika ushindani baada ya mwanzo mbaya wa kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026.

Related Posts